Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa COP20 Lima ni lazima uweke historia:UNFCCC

Katibu Mtendaji wa UNFCCC Christiana Figueres akifungua mkutano wa COP20 huko Lima, Peru. (Picha:COP20)

Mkutano wa COP20 Lima ni lazima uweke historia:UNFCCC

Katibu mtendaji wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya mkataba kuhusu makubaliano ya tabianchi, UNFCCC, Christiana Figueres ametaja mambo makuu manne ambayo yanapaswa kukamilishwa ifikapo mwishoni mwa mkutano wa 20 kuhusu mabadiliko ya tabianchi, COP20 huko Lima, Peru tarehe 12 mwezi huu.

Akifungua mkutano huo ametaja mambo hayo kuwa ni rasimu ya makubaliano ya dunia inayobainisha mchango ya kila nchi na ambayo itawasilishwa mwakani na pili ni kuimarisha maendeleo ya hatua zinazochukuliwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi sambamba na zile za kupunguza makali ya athari za mabadiliko hayo.

Jambo la tatu ni kuchagiza usaidizi wa kifedha kwa nchi zinazoathiriwa zaidi na mabadiliko hayo na nne ni kuongeza kasi ya wadau katika utekelezaji wa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Bi. Figueres amesema ni vyema mkutano huo wa Lima ukaweka historia kwa kuwa na mipango ya kudumu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.