Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shinikizo dhidi ya watetezi haki Burundi linanitia hofu: Mtaalamu

UN Photo - Jean-Marc Ferre
Michel Forst, Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu watetezi wa haki za binadamu Picha:

Shinikizo dhidi ya watetezi haki Burundi linanitia hofu: Mtaalamu

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu watetezi wa haki za binadamu Michel Forst amehitimisha ziara yake nchini Burundi na kuitaka serikali kuacha kubinya uhuru wa watetezi wa haki za binadamu.

Akizungumza mjini Bujumbura, Burundi Bwana Forst ameeleza masikitiko yake juu ya madhila wanayokumbana nayo watetezi wa haki za binadamu nchini humo akisema wanachukuliwa kama wapinzani wa kisiasa.

Amesema kiuhalisia watetezi hao wanaendeleza na kulinda haki za kibinadamu na uhuru wa kiraia.

Hata hivyo ameelezea kuguswa na vile ambavyo mashirika yasiyo ya kiraia yanavyotekeleza majukumu yao kwa weledi licha mazingira magumu wanamofanyika kazi.

Bwana Forst pia amesisitiza kuwa vitisho na Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeitaka serikali ya Burundi kulegeza shinikizo lake dhidi ya watetezi wa haki za binadamu nchini humo.

Halikadhalika amesema ameieleza serikali ya Burundi juu ya hofu yake kuhusu sheria kuhusu uhuru wa vyombo vya habari akisema ziko kinyume na matakwa ya kimataifa.

Ripoti kamili ya ziara ya mtaalamu huyo nchini Burundi itawasilishwa mbele ya Baraza la haki za binadamu.