Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fikra potofu dhidi ya matumizi ya choo zitokomezwe:UM

Mwananchi akijenga choo hapa ni Cambodia. (Picha:UNICEF-Cambodia)

Fikra potofu dhidi ya matumizi ya choo zitokomezwe:UM

Tarehe 19 mwezi Novemba kila mwaka ni siku ya vyoo duniani. Siku hii imetengwa kwa ajili ya kuchukua hatua na kuhamasisha uelewa kuhusu watu ambao hawana vyoo, hii ikiwa ni haki ya kila mwanadamu. Mwaka huu, kauli mbiu ya siku hii iliyotambuliwa rasmi na Baraza Kuu mwaka 2013, ni usawa na hadhi. Kampeni inalenga kuchagiza juhudi za kumaliza vitendo vya kujisaidia hadharani na kumulika jinsi upatikanaji wa huduma za mazingira safi unaweza kupunguza visa vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Takwimu zinaonyesha kwamba kati ya watu bilioni saba duniani watu 2.5  hawana vyoo vya kutosha na kati yao bilioni 1 hujisaidia haja kubwa katika eneo lililo wazi, mathalani katika mashamba, misitu, au vyanzo vya maji. Basi ungana na Assumpta Massoi katika ripoti hii.