Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apongeza IGAD kwa hatua za kukomesha mgogoro Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon. (Picha:UN/Maktaba)

Ban apongeza IGAD kwa hatua za kukomesha mgogoro Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amepongeza misimamo imara iliyopitishwa na wakuu wa nchi wanachama wa  jumuiya ya maendeleo IGAD kuhusu mgogoro wa Sudan Kusini kwa maslahi ya wananchi

Tarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu inasema ametiwa moyo na  dhamira ya pande kinzani kusitisha mapigano na kufikia makubaliano kuhusu mgawanyo wa madaraka jumuishi ndani ya siku 15.

Imemnukuu Bwana Ban akisema ana matumaini kuwa pande hizo zitasimamia ahadi zao kuhusu amani na kujihusisha katika majadiliano kwa dhati  ili kufikia makubaliano ya kina ya amani yatakayoshughulikia chanzo cha mgogoro Sudan Kusini