Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu apongeza makubaliano ya serikali ya kitaifa Yemen

Katibu Mkuu Ban Ki-moon.Picha ya UM/NICA

Katibu Mkuu apongeza makubaliano ya serikali ya kitaifa Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tangazo la uundwaji wa serikali ya amani na umoja wa kitaifa nchini Yemen, na kuwapongeza Rais Abd Rabbu Mansour Hadi na waziri mkuu mteule kwa uongozi wao katika mchakato huo.

Kwa mujibu wa msemaji wa Katibu Mkuu, Bwan Ban pia amepongeza pande katika makubaliano hayo kwa kuahidi  kukubali mamuzi ya Rais na Waziri Mkuu na kuendelea kuunga mkono serikali mpya.

Katibu Mkuu amesema tangazo hilo ni hatua kuelekea amani na  ntulivu nchini humo hususani ni wakati huu ambapo kumekuwa na sintofahamu nchini Yemen.

Amezikumbusha pande zilizohusika juu ya ahadi zao za makubaliano waliyotia saini kwa ajili ya serikalia ya amanina umoja wa kitaifa. Amesema Yemen inakumbuna na changamoto kubwa kwa sasa ambayo yaweza kutatuliwa kwa pande zote kufanya kazi pekee kwa masalahi ya nchi na kutekeleza makubaliano bila kuchelewa.

Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa unatarajia kuendelea kushirikiana na Rais, Waziri Mkuu, serikali na viongozi wote wa Yemen kaika kutafuta kujenga nchi yenye  demokrasia inayojali mahitaji  ya watu wake.