Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpigano yaendelea Darfur, mamlaka Sudan zatakiwa kulinda raia na watoa misaada

Mpigano yaendelea Darfur, mamlaka Sudan zatakiwa kulinda raia na watoa misaada

Mamlaka nchiniSudanzimetakiwa kuchukua hatua mathubuti kulinda raia na wafanyakazi wa misaada ya kiutu wakati huu ambapo machafuko yanaendeleaDarfur

Wito huo umetolewa na maafisa wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika ambao wamesema wanasononeshwa na kuendelea kwa machafuko katika ukanda huo.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema  mwakilishi maalum wa ujumbe wa pamoja wa muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur  Joseph Mutaboba pamoja na mwakilishi mkazi  na mratibu wa misaada ya kiutu Sudan Ali Al-Za'tari wamesema katika taarifa yao kuwa zaidi ya watu laki mbili wamepoteza makazi tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Amesema taarifa hiyo inasema jamii ya watoa misaada inazuiwa kuwafikia waathiriwa wa machafuko jambo linalosababisha hata idadi ya waliopoteza makazi kutofahamika kirahisi

Maelfu ya watu wamepoteza makazi hukoDarfurtangu kuzuka kwa mapigano mwaka 2003 kati ya vikundi vya waasi na vikosi vya serikali na wapiganaji wanaofahamika kwa jila la Janjaweed.

Ujumbe wa pamoja wa muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa (UNAMID) unasaidia katika kulinda raia na kusaidia katika mazungumzo ya upatanisho ili kutafuta suluhisho la kisiasa.