Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Facebook yaongeza kitufe cha kurahisisha kuchangia makabiliano ya Ebola

UN Photo/Ari Gaitanis
Picha:

Facebook yaongeza kitufe cha kurahisisha kuchangia makabiliano ya Ebola

Tukisalia katia afya, Kampuni ya habari ya kijamii, Facebook, imetangaza kuwa inaongeza kitufe kitakachorahisisha watumiaji wake kutoa mchango kwa mashirika yanayojikita katika kupambana na homa ya Ebola.

Taarifa iliyotolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia dharura ya Ebola, UNMEER, imesema kwamba katika wiki moja ijayo, watumiaji wa Facebook wataweza kuona na kubonyeza kitufe cha kuchangia shirika la International Medical Corps, Mashirika ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyenkundu, na shirika la Save the Children.

Facebook imesema kuwa imechagua mashirika yanayofanya kazi moja kwa moja mashinani, na ambayo yanaweza kukubali fedha kutoka kote duniani.

Kampuni hiyo pia inachangia na kupeleka mitambo 100 ya mawasiliano ya satellite kwa maeneo yaliyoathiriwa, ili kuboresha huduma za intanet.