Madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa kilimo na biashara yajadiliwa
Mjadala wa uwiano kati ya mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula, kilimo na biashara umefanyika mjini Bujumbura Burundi ukiwaleta pamoja wataalamu wa sekta hizo kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wanadiplomasia na watunga sera.
Mjadala umefanyika ikiwa ni takribani mwezi mmoja na Nusu baada ya kikao cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambacho kiliangazia mabadiliko ya tabia nchi duniani , ikiwamo mipango na malengo ya kunusuru sayari dunia katika madhara yatokanayo nayo. Washiriki wameangazia jinsi ya kuweka sera zenye uwiano kwa sekta tajwa. Mathalani utekelezaji wa lengo namba Moja la maendeleo ya milenia la kupunguza umaskini ambalo lapaswa lisiathiri mazingira.
Halikadhalika hoja ya viwanda visivyoathiri mazingira isiathiri usalama wa chakula au uzalishaji viwandani.
Lakini nini ilikuwa maazimio ya ya mkutano huo? Na zaidi walengwa yaani wakulima na wale wanaofanya shughuli zinazohatarisha mazingira wana mtazamo gani? Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga amevinjari mkutanoni na kwa wananchi na kituandalia taarifa ifuatayo.