Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yawapigia chepuo wanawake wa Libya kuhusu katiba

Picha: NICA

UN yawapigia chepuo wanawake wa Libya kuhusu katiba

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na taasisi zake zimeendesha mafunzo maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake wa Libya ambao baadhi yao kwa sasa wapo katika hali ngumu kutokana na machafuko yanayoendelea.

Umoja huo wa Mataifa umewaleta pamoja wanawake nchini Libya na kuwafungulia njia kuhusiana na matakwa ya Katiba mpya ambayo itazingatia maslahi ya wanawake.

Mkutano huo uliofanyika kati ya Novemba mosi na nne uliwaleta pamoja zaidi ya wanawake 60 kutoka maeneo mbalimbali. Pia mkutano huo uliofanyika Cairo, Misri ulihudhuria na wataalamu kutoka Baraza la Uandikaji Katiba.