Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waataalamu wazitaka nchi kutekeleza maazimio ya CEDAW

UN Photo/Albert Gonzalez Farran
Picha:

Waataalamu wazitaka nchi kutekeleza maazimio ya CEDAW

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa, Kamati mbili za umoja huo zinazohusika na haki za binadamu zimeunganisha nguvu  na kuanisha kinagaubaga majukumu ambayo yanapaswa kuchukuliwa na nchi wanachama kwa ajili ya kutokomeza vitendo hatarishi dhidi ya wanawake na wasichana. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Taarifa ya George Njogopa)

Kamati hiyo inayoundwa na jopo la wataalamu waliobobea katika masuala ya haki za binadamu imeanisha vitendo hivyo pamoja na kukeketa wanawake,mitaala na ndoa za utotoni pamoja na zile zinazofanywa pasipo ridhaa ya mhusika.

Kutafsiri kwa mkakati huo ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo maazimio ya kimataifa ikiwamo maazimuo yaliyofikiwa miaka kadhaa ya nyuma ambayo yalihimiza dunia kutokomeza vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Mkataba huo wa kimataifa ambao unafahamika kitaalamu kama CEDAW uliasisiwa wakati wa mkutano wa kimataifa wa wanawake uliofanyika Beijing, China miaka kadhaa iliyopita.

Mmoja wa wataalamu walioshiriki kutafsiri mkakati huo Bi Violeta Neubauer amesema kuwa wanawake wananadamwa na matukio mengi ambayo yanawarudisha nyuma kupata haki zao za msingi.

Amesema kuwa miongoni mwa matukio hayo yamejificha chini ya mgono wa kimila, tamaduni za kidini ama mapokeo mengine ya kijamii ambayo kwa msingi yamelenga kumkandamiza mwanamke.