Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lapitisha azimio la kupinga biashara ya mkaa Somalia

UN Photo/Tobin Jones)
Lori lililobeba mkaa imepinduka kwenye barabara kutoka Afgooye kwenda Baidoa. Picha:

Baraza la Usalama lapitisha azimio la kupinga biashara ya mkaa Somalia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limepitisha azimio la kulaani uuzaji wa mkaa nje ya Somalia, ambao unakiuka marufuku iliyowekwa kabisa kwa biashara hiyo nchini humo.

Baraza la Usalama pia limezitaka nchi wanachama, zikiwemo zile zinazochangia walinda amani Somalia, AMISOM, kuheshimu na kutekeleza majukumu yao ya kuzuia biashara ya mkaa  kama ilivyowekwa kwenye azimio namba 2036 la Baraza hilo.

Baraza hilo limelaani kuendelea kuliuzia kundi la kigaidi la Al-Sahabaab na makundi mengine yaliyojihami, na kuongeza kupiga marufuku uagizaji na uuzaji wa mkaa nje ya Somalia, na pia kuongeza muda wa vikwazo vya uagizaji silaha nchini humo.

Mwakilishi wa Kudumu wa Somalia kwa Umoja wa Mataifa, ameongea baada ya kupitishwa azimio hilo.

"Tunakaribisha idhinisho la vyombo vya usalama baharini kuzuia usafirishaji na biashara ya magendo ya mkaa unaouzwa nje na ndani ya Somalia na pia tunakaribisha idhinisho la wanajeshi wa majini wa kimataifa kupokonya silaha zinazosafirishwa kwenda kwa vikosi visivyo vya serikali ya Somalia"