Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili hali Palestina na Mashariki ya kati

Kikao cha Baraza la Usalama.(Picha ya UM/Rick Bajornas)

Baraza la usalama lajadili hali Palestina na Mashariki ya kati

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili hali Mashariki ya kati  hususani Palestina . Grace Kaneiya anaarifu zaidi.

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Akiongea katika kikao hicho Katibu Mkuu Ban Ki Moon amesema kilio chake ni kwa jumuiya ya kimataifa kunusuru hali ya kibinadamu huko Gaza ambako amesema raia wanaendelea kupata madhila kutokana na sintofahamu kati ya taifa hilo na Isarel na kusema kuwa suluhisho la kisiasa ndiyo muarubaini .

(SAUTI BAN)

"Dola milioni mia nne kumi na nne zinahitajika haraka kwa ajili ya misaada ya kibinadamu, huku dola bilioni mbili zikihitajika kwa ajili ya ujenzi mpya wa Gaza. Zaidi ya wakazi laki moja wa Gaza hawana makazi huku zaidi ya elfu 50 wakijihifadhi katika majengo ya shule za UNRWA".

Kuhusu Syria na Lebanon Ban amezitaka pande zinazokinzana kuhakikisha ulinzi wa raia na kutaka ukanda huo kumpa ushirikiano wa kutosha mwakilishi maalum katika kufikia suluhu la kisiasa katika ukanda huo.