Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yatoa ripoti kuhusu madhila yanayowakumba wahamiaji

Picha: IOM

IOM yatoa ripoti kuhusu madhila yanayowakumba wahamiaji

Shirika la kimataifa la wahamiaji IOM limechapisha ripoti yake inayonyesha madhila wanayokumbaana wahamiaji ambao baadhi yao wamepoteza maisha wakati wakiwa safarini.

Likionyesha idadi kubwa zaidi ya watu waliopoteza maisha  IOM limetoa wito ikitaka kuchukuliwa juhudi za pamoja za kukabiliana na janga hilo linaloendelea kuwakumba wahamiaji wengi.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kiasi cha wahamiaji 40,000 walipoteza maisha katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000 na kuelekeza kuwa idadi hiyo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa.

Ripoti hiyo iliyochapishwa katika kurasa 200 imehusisha pia tukio la Oktoba 2013 ambapo wahamiaji zaidi ya 400 walipoteza maisha katika kisiwa cha Lampedusa wakati wakisafiri kuelekea Italia.