Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ebola ni kiashiria cha moja ya changamoto zinazoendelea kukumba Afrika:Zuma

UN Photo/Cia Pak
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini akihutubia Baraza Kuu. (Picha:

Ebola ni kiashiria cha moja ya changamoto zinazoendelea kukumba Afrika:Zuma

Ugonjwa wa Ebola umeendelea kutawala hotuba za wakuu wa nchi na serikali wanaohutubia mjadala wa wazi wa mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo hotuba ya hivi karibuni zaidi ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini imesema mlipuko huo umefichua moja ya changamoto kubwa inazoikumba Afrika.

Rais Zuma amesema hayo wakati huu ambapo shirika la afya duniani, WHO limesema hadi sasa sasa watu walioambukizwa Ebola tangu uzuke mwezi Machi ni 5,843 huku 2,803 wakifariki dunia.

(Sauti ya Rais Zuma)

“Tunaamini kuwa Ebola ungalikuwa umedhibitiwa ndani ya siku chache, iwapo ungalikuwa umelipuka nchi zilizoendelea. Lakini umekuwa mlipuko na kutishia uchumi wa nchi za Afrika zilizokumbwa na mlipuko. Mlipuko umefichua changamoto za uwezo na ukosefu wa miundombinu na uhaba wa rasilimali nyinginezo barani Afrika.”

Rais Zuma amezungumzia pia malengo ya maendeleo ya milenia akisema Afrika Kusini imetimiza lengo namba mbili la elimu kwa wote huku lile la kwanza kuhusu njaa na lilkiwa limepunguzwa kwa asilimia hamsini.