Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wauaji wa wahamiaji wakumbane na mkono wa sheria :UM

UN Photos/ Paulo Filgueiras
Mwana Mfalme Zeid al Hussein @

Wauaji wa wahamiaji wakumbane na mkono wa sheria :UM

Kamishna mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa  Zeid Ra’ad Al Hussein,  ameitaka Misri na nchi nyingine za kaskazini mwa Afrika na Ulaya ambazo zina taarifa zenye taarifa sanifu kufanya juhudi za kuwafikisha katika vyombo vya sheria wasafirishaji  haramu wanaotuhumiwa kuzamisha kwa makusudi mashua na kusababisha vifo vya wakimbizi na wahamiaji kati ya watu 300 hadi 500 katika bahari ya Mediterranian wiki iliyopita.

Taarifa ya kamishna mkuu huyo imesisitiza kuwa ni muhimu kukomesha hali inayoendelea ya kutojali sheria katika matukio hayo na kuongeza kuzitaka nchi husika kutafuta chanzo kinachosukuma watu kufanya safari hizo hatari ili zinazosababisha matukio kama hayo.

Bwana Zeid pia ametaka hatua kama hizo zichukuliwe na nchi nyingine ili kukomesha uhalifu wa jinsi hiyo sehemu nyingine duniani ikiwemo ghuba ya Edeni, bahari ya Hindi na Caribbean pamoja na wale ambao husafirisha wahamiaji kupitia njia za barabara.

Ametaka nchi husika bila kujali ikiwa raia waliokufa ni wanchi zao au la kuagiza vikosi kamili vya askari na mifumo ya kisheria katika uchunguzi huo akisisitiza kuwa ni watuhumiwa wachache ambao huuwa , hubaka au kuwapora wahamiaji katika misafara yao na kuchukuliwa hatua za kisheria.

"Kamishna Mkuu anasema kitendo katili cha kuzamisha kwa makusudi mashua iliyo na mamia ya watu wanyonge ni uhalifu ambao ni lazima uadhibiwe. Kama taarifa za waathirika ni kweli – na zinaonekana ni za kuaminika - tunayaona haya kama mauaji ya halaiki katika bahari ya Mediterranenia."