Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani ya Darfur yajadiliwa Qatar

UN Photo/Paulo Filgueiras
Mohamed Ibn Chambas, Mwakilishi wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika. Picha:

Amani ya Darfur yajadiliwa Qatar

Kumekuwa na hatua kubwa ya utanzuaji wa mzozo wa Darfur nchini Sudan kufuatia majadiliano yaliyofanyika huko Doha, Qatar yakimhusisha pia mpatanishi wa mzozo huo Momahed Chambas.

Majadiliano hayo ambayo yana shabaha ya kutanzua mzozo huo uliodumu kwa muda mrefu yaliwajumuisha pia viongozi wa ngazi mbalimbali  akiwemo Naibu Waziri Mkuu wa Qatar Ahmed bin Abdulah na Mwenyekiti wa jopo la wazee wa Umoja wa Afrika Thabo Mbeki.

Wote wameunga mkono hatua iliyoanzishwa na Rais Omer Al-Bashir ya kuanzisha maridhiano ya kitaifa kwamba mpango huo utafanikisha amani katika jimbo hilo.