Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wasaidia kulinda haki za binadamu kwenye Intaneti

UN Photo/Evan Schneider
Thomas Gass, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia uratibu wa sera. Picha:

Umoja wa Mataifa wasaidia kulinda haki za binadamu kwenye Intaneti

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia uratibu wa sera amesema intaneti inafaa iwe wazi, huru, salama na ya kuaminika.

Thomas Gass amsema kufanikisha kwa malengo haya ndilo mojawapo ya lengo la mkutano wa usimamizi wa intaneti uliofanyika Istanbul Uturuki 2-5 Septemba.

Tangu mwaka wa 2006, kila mwaka mkutano huu unaandaliwa ili kujadili jinsi ya kuwezesha intaneti endelevu, iliyo imara, salama, tulivu na ya kuendelea .

Gass anaelezea jinsi kuunganishwa kwa mabara kutachangia katika kuimarisha utawala wa intaneti.

(Sauti ya Gass)