Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yasaka muongozo wa tiba dhidi ya Ebola

Harakati za kudhibiti Ebola nchini Guinea-Conakry. Picha @WHO

WHO yasaka muongozo wa tiba dhidi ya Ebola

Wakati mkutano wa kamati ya dharura ya shirika la afya duniani WHO kuhusu mustakhbali wa Ebola ukiingia siku yake ya pili, Shirika hilo limesema mapema wiki ijayo litaitisha kikao cha jopo la wataalamu wa maadili ya kitabibu kuhusu majaribio ya tiba dhidi ya ugonjwa huo huko Afrika Magharibi. Amina Hassan na taarifa kamili.

(Taarifa ya Amina)

Mkurugenzi Msaidizi wa WHO Marie-Paule Kieny amesema kwa sasa hakuna dawa iliyosajiliwa au chanjo dhidi ya kirusi cha Ebola lakini kuna mbinu kadhaa zinazoendelezwa ambazo zinaweza kuwa na jibu.

Amesema hatua hiyo inatokana na kuibuka kwa mjadala kufuatia matibabu ya hivi karibuni ya Ebola wataalamu wa afya wa shirika la Samaritan, matibabu yaliyofanyika kwa kutumia dawa ya majaribio.

Mjadala huo ni iwapo dawa hiyo ambayo haijafanyiwa majaribio lakini kutoa tiba inaweza kuwa salama na kutumika kwenye mlipuko kwa kuzingatiwa kiwango kidogo kilichopo na iwapo itatumika ni nani apatiwe.

Amesema wanahitaji kuuliza wataalamu hao ili wapate muongozo wa kile kinachofaa kufanyika.