Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yatiwa wasiwasi na ghasia zinazoendela Lebanon

UN Photo/Paulo Filgueiras
Ross Mountain, Mratibu wa Hahaki za Binadamu. Picha@

UM yatiwa wasiwasi na ghasia zinazoendela Lebanon

Kaimu Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, Ross Mountain, amelaani vikali mashambulizi dhidi ya jeshi la Lebanon na mapigano yanayoendelea kwenye maeneo ya Arsal.

Mashambulizi hayo yamesababisha askari 16 na raia zaidi ya sita kufariki dunia, pamoja na watu wengine kujeruhiwa.

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa amepeleka rambirambi zake kwa familia za wahanga akiwatakia nafuu majeruhi.

Ameongeza kwamba, Umoja wa Mataifa unaendelea kuliunga mkono jeshi la Lebanon katika juhudi zake za kuleta usalama na utulivu nchini humo .

Serikali za mitaa zinakadiria kwamba takriban familia 3,000 za Arsal zimekimbia makwao kutokana na ghasia. Juu ya hayo, zaidi ya wakimbizi 100,000 kutoka Syria wamepata hifadhi katika mji huo.

Ross Mountain, ambaye pia ni Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu nchini humo, alikuwa ameonya awali kuhusu hatari ya mvutano baina ya wakimbizi wa Syria na raia wa Lebanon.