Bado nyuklia, maji na makaa ya mawe ni muhimu kwa nishati Afrika:

4 Agosti 2014

Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim amesema vyanzo vya nishati vya maji, nyuklia na makaa ya mawe ni muhimu kwa bara la Afrika linaoibukia hivi sasa.

Amesema hayo katika mjadala unaoendelea huko Washington D.C kuhusu Afrika inayoibuka.

(Sauti ya Kim)

"Iwapo tutajikuta katika mazingira ambapo tunakataa makaa ya mawe, nyulia na hata nishati itokanayo na maji, basi tutakuwa kweli tunajidanganya."

Amesema wanachofanya sasa ni kudhibiti uharibifu wa mazingira utokanao na ujenzi wa mabwawa na kuheshimu haki za wazawa na wakazi wa eneo husika.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter