Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baharia amekuletea nini? IMO yasaka jibu kupitia mitandao ya kijamii

Picha@IMO

Baharia amekuletea nini? IMO yasaka jibu kupitia mitandao ya kijamii

Leo tarehe 25 Juni ni siku ya mabaharia duniani ambapo ujumbe wa siku hii ni kutafakari mchango wa mabaharia ulimwenguni wakati huu ambapo shirika la kimataifa la masuala ya bahari, IMO likisema mchango wao haupewi umuhimu unaoustahili.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa hii, Naibu Mkurugenzi wa  IMO Juvenal Shiundu amesema lengo la kuchagua ujumbe huo.

(Sauti ya Juvenal-1)

Bwana Juvenal anaelezea kampeni ya mwaka huu ya kufahamu kutoka kwa wananchi mchango wa mabaharia kwenye maisha yao.

(Sauti ya Juvenal-2)

IMO imehoji iwapo mtu amewahi kufikiria majukumu ya mabaharia katika usafirishaji wa bidhaa zinatotumika kila siku na kuwashukuru kwa utendaji wao.