Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ziarani Namibia, baadaye kuelekea Equitorial Guinea na Kenya

Ban ziarani Namibia, baadaye kuelekea Equitorial Guinea na Kenya

03hapanapalebansafariniafrika

Katibu Mkuu wa Umjoja wa Mataifa Ban Ki-Moon anaelekea nchini Namibia ambako pamoja na mambo mengine atashiriki ufunguzi rasmi wa jengo la Umoja wa Mataifa kwenye mji mkuu Windhoek.

 Jengo hilo litakuwa makao makuu mashirkia 12 ya Umoja wa Mataifa na miradi yake nchini Namibia. Bwana Ban pia atakuwa na mazungumzo na viongozi wa serikali akiwemo Rais Hifikepunye Pohamba.

Katibu Mkuu ataondoka Namibia hapo jumatano akielekea Malabo nchini Equitorial Guinea, kuhudhuria mkutano wa Muungano wa Afrika AU.

Hatimaye atakwenda Nairobi , Kenya ambapo atashiriki shughuli ya kufunga rasmi Mkutano wa Baraza la Umoja wa Maitaifa kuhusu Mazingira, UNEA ulioanza leo.