Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua muongo wa nishati endelevu kwa wote; Tanzania yaweka bayana mipango yake

Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini Tanzania. @Radio ya UM

UM wazindua muongo wa nishati endelevu kwa wote; Tanzania yaweka bayana mipango yake

Hatimaye Umoja wa Mataifa umezindua muongo wa nishati endelevu kwa wote wenye lengo la kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030 basi kila mkazi wa sayari hii atakuwa na nishati ya umeme. Kupitia mpango huo vyanzo vya nishati hiyo vinawekwa bayana wakati huu ambapo wana mazingira nao wako makini ili miradi hiyo isihatarishe uwepo wa dunia hii. Miongoni mwa nchi zilizoshiriki ni Tanzania ambayo pia imepata heshima ya kuwakilisha bara la Afrika kupitia mradi huo. Je ni kwa vipi na manufaa ya mradi ni yapi? Basi Ungana na Assumpta Massoi katika mahojiano yake na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ambaye anaanza kwa kuzungumzia ujumbe wa Tanzania..