Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dkt Salim azungumzia uongozi Afrika na mustakhbali wa Sudan Kusini

Dkt Salim azungumzia uongozi Afrika na mustakhbali wa Sudan Kusini

Mwaka 2013 umefikia ukomo. Barani Afrika, mengi yametokea na mengine yanaendelea kutokea. Mathalani kifo cha Mzee Madiba na mzozo unaoendelea Sudan Kusini na kufanya wanadiplomasia kuendelea kukuna vichwa vyao kila uchao kupata suluhu ya kudumu za mzozo huo ndani ya taifa hilo changa lililopaswa kuwa mfano. Je nini mustakhbali wa Afrika baada ya Mandela? Na vipi Sudan Kusini?. Assumpta Massoi wa Idhaa hii alifanya mahojiano kwa njia ya simu na  Mwanadiplomasia wa muda mrefu Katibu Mkuu Mstaafu wa uliokuwa Umoja wa nchi  huru za Afrika, OAU sasa AU Dokta Salim Ahmed Salim kuhusu masuala hayo.