Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jitihada za vijana kujihusisha katika nafasi za maamuzi

Jitihada za vijana kujihusisha katika nafasi za maamuzi

Siku ya kimataifa ya vijana ambayo huadhimishwa kila Agosti 12 hulenga kuangalia ustwawi wa kundi hilo katika nyanja ya kijamii, kiuchumi, masuala ya elimu, afya na mengineyo.Mwaka huu maudhui ni ushiriki wa vijana katika masuala ya kisiasa.

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau wa maendeelowanasema ushiriki wa vijana ni muhimu katika maendeleo endelevu. Katibu Mkuu Ban Kin-moon katika ujumbe wake amewataka vijana kupaza sauti, huku akiwataka viongozi wawasikilize. Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana Ahmad Alhendawi anasema vijana wanaweza kuleta mabadiliko.

(SAUTI ALHENDAWI)

‘‘Nimekutana na vijana kutoka maeneo tofauti, wakiwa na fursa sahihi wanaweza kubadili masiha ya baadaye, Sio tu viongozi wa siku zijazo lakini ni viongozi wa sasa. Vijana wana mchango mkubwa katika maendeleo na wana nafasi kubwa."

Je? nchini Tanzania ambapo maadhimisho hayo yalifanyika jijini Dar es salaama vijana wanasemaje kuhusu kutumia fursa za kisisasa na kiuchumi kwa ajaili ya maendeleo / Tuungane na Grace Kaneiya.