Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki ya mtoto ya kucheza yatimia huko Libya

Haki ya mtoto ya kucheza yatimia huko Libya

Nchini Libya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na serikali limefungua kituo cha kwanza kati ya 13 vya michezo ya watoto na hivyo kuweka mazingira rafiki na salama kwa kundi hilo kutimiza moja ya haki yao ya msingi ya kucheza kama sehemu muhimu ya kuimarisha makuzi yao.

UNICEF inasema hatua ya leo ambayo ni sehemu ya usaidizi wa kibinadamu baada ya mapinduzi ya mwaka 2011 nchini humo, ni muhimu kwa kuzingatia Libya ina sehemu chache za watoto kucheza na hata zilizopo si salama.

Kituo hicho kilichopo eneo la Abu slim kwenye mji mkuu Tripoli kinafanya kazi na kuleta tabasamu na furaha kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka Mitatu hadi Kumi na moja.