Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapambano dhidi ya ukeketaji Tanzania, safari ni ndefu lakini kuna matumaini.

Mapambano dhidi ya ukeketaji Tanzania, safari ni ndefu lakini kuna matumaini.

Dunia ikiwa inaadhimisha siku ya kupinga ukeketaji kwa wanawake na wasichana inaelezwa kuwa mila na desturi ni kikwazo kikubwa katika harakati za kutokomeza vitendo hivyo.

Katika mahojiano na Joseph Msami wa  idhaa hii Mtaalamu wa masuala ya jinsia kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA nchini Tanzania, Christine Kwayu amesema licha ya mila hizo UNFPA kwa kushirikiana na wadau wanajitahidi kuelimisha jamii ili kuondokana na ukeketaji. Bi Kwayu kwanza anaanza kwa kueleza juhudi za shirika hilo katika kutokomeza ukeketaji nchini humo.

(SAUTI MAHOJIANO)