Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini imetakiwa kukabiliana na chanzo cha machafuko:

Sudan Kusini imetakiwa kukabiliana na chanzo cha machafuko:

Serikali ya Sudan Kusini imetakiwa na Umoja wa Mataifa kukabiliana na mizizi ambayo ni chanzo cha vita vinavyoendelea ili kuleta amani katika taifa hilo changa. Sudan Kusini inashuhudia machafuko ya ndani ynayoendelea baada ya majeshi yanayomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais kubeba silaha na kuanza kupambana na serikali mwishoni mwa Desemba mwaka jana.

Akizungumza mjini Juba wakati wa mwisho wa ziara yake ya siku mbili mkuu wa operesheni za kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Herve Ladsous amesema ni lazima kusitisha mapigano.

(SAUTI YA HERVE LADSOUS)

"Tunatumai kwamba machafuko haya yanaweza kudhibitiwa, kwanza kwa kufanikiwa kusitisha mapigano mkataba uliotiwa saini 23 Januari, lakini pia kwa kutafuta njia za kushughulikia chanzo cha hali hii mbaya"

Wanajeshi wa ziada wa kulinda amani wanatarajiwa kupelekwa kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS . Desemba mwaka jana baraza la usalama liliidhinisha ongezeko la muda la wanajeshi na polisi 13,000 na wanajeshi wa ziada watapelekwa kuungana na wa sasa 7000.