Ukosefu wa choo ni jambo la kudhalilisha: Eliasson

17 Novemba 2013

Ni jambo la kudhalilisha na lisilokubalika ya kwamba watu bilioni Mbili na Nusu duniani hawana huduma bora za vyoo na huishia kujisaida hovyo na kuhatarisha afya zao na za jamii zao. Ni kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson katika kuelekea kuadhimisha siku ya choo duniani tarehe 19 Novemba.

(Sauti ya Jan Eliasson)

“Ni jambo lisilokubalika kimaadili, kiafya, kwa haki za binadamau na hata kiuchumi. Kwa sababu hii ina maana kwamba nchi zitakuwa na tatizo la kudumu la kiafya na ukosefu wa ajira kutokana na suala hili la kutisha la kukosa huduma za kujisafi na vyoo.”

Bwana Eliasson amesema ni lazima kuchukua hatua na kwamba hakuna mtu mmoja anaweza kufanya kila kitu lakini kuna kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya ili kuondokana na adha hiyo