Matokeo makubwa Sasa, kuchagiza maendeleo Tanzania:

9 Oktoba 2013

Mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu ufadhili na maendeleo umehitimishwa mjini New York, Marekani ambapo Tanzania ikiwa moja ya nchi shiriki ilieleza bayana hali inayoendelea nchini humo kufadhili yenyewe shughuli za maendeleo wakati huu ambapo ufadhili wa kigeni unasuasua. Je ni hatua gani serikali inachukua kutekeleza shughuli hizo ikiwemo malengo ya maendeleo ya milenia? Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania Mahadhi Juma Maalim aliweka bayana katika mazungumzo yake na Flora Nducha na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa. Anaanza kwa kubainisha kile walichoeleza kwenye mjadala huo.