Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria inakwaza ajira za mabaharia: Nahodha Mlesa

Sheria inakwaza ajira za mabaharia: Nahodha Mlesa

Ikiwa Juni 25 ni siku ya kimataifa ya mabaharia, Umoja wa Mataifa umezungumzia umuhimu wa zaidi ya mabaharia Milioni Moja na nusu duniani kote ambao huwezesha kusafiri salama kwa shehena mbali mbali baina ya mabara, nchi na maeneo. Hata hivyo mabaharia hao hukumbwa na mikasakamavile uharamia, vimbunga na kadhalika ali mradi misukosuko baharini. Na zaidi ya hapo ajira nazo zinatajwa kuwa changamoto licha ya kuwa na stadi na elimu zinazotakiwa. William Mlesa, mhadhiri mwanamizi katika chuo cha majini Tanzania, DMI alianza ubaharia mwaka 1965 akiwa na umri wa miaka 19 na akapanda cheo hadi unahodha wa meli kubwa zisizo na mipaka. Katika mahojiano na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa Walesa amezungumzia mambo kadha wa kadha ikiwemo changamoto za ubaharia. Lakini hapa anaanza kwa kuzungumzia vile anavyopokea siku hii ya kimataifa ya mabaharia.