Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Quinoa zao la kumkomboa mkulima, lastahimili ardhi kame!

Quinoa zao la kumkomboa mkulima, lastahimili ardhi kame!

Hatimaye mwaka wa kimataifa wa zao la Quinoa umezinduliwa rasmi kwenye kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Shughuli hiyo imeshudiwa na viongozi na wawakilishi wa mataifa na mashirika mbali mbali akiwemo Rais wa Bolivia, Evo Morales ambaye nchi yake ndiyo inaongoza duniani kwa kuuza zao hilo nje ya nchi. Tayari tumeelezwa kuwa zao la Quinoa, ambayo ni nafaka itokanayo na mbegu za mmea huo jamii ya spinachi, limeenea nchi mbali mbali duniani ikiwemo Kenya na kutoa matumaini ya kutokomeza njaa na umaskini miongoni mwa wakulima. Basi kwa taarifa zaidi kuhusiana na zao hilo na manufaa yake fuatana na Assumpta Massoi katika ripoti hii maalum.