Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake tusiporomoshane! Tushirikiane ili tusonge mbele: Dokta Chuwa

Wanawake tusiporomoshane! Tushirikiane ili tusonge mbele: Dokta Chuwa

Harakati za kukomboa wanawake zianze na wanawake wenyewe kwa kuweka ushirikiano zaidi badala ya kuhujumiana, amesema Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania Dkt. Albina Chuwa alipoulizwa na Idhaa hii kuhusu ujumbe wa siku hii wa Usawa kwa wanawake ni maendeleo kwa wote! Dokta Chuwa ambaye ni mtakwimu wa kwanza wa Taifa mwanamke kwa Afrika Mashariki amesema mustkhabali kwanza uanze kwa wanawake wenyewe. Hapa anataja kwanza fursa zilizomwezesha kufika hapo alipo….