Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP21 yaanza leo huko Paris, Ufaransa

COP21 yaanza leo huko Paris, Ufaransa

Hatimaye mkutano wa 21 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP21 unaanza leo huko Paris, Ufaransa, ukileta pamoja viongozi zaidi wapatao 150.

Lengo la mkutano huo ni kupitisha makubaliano ambayo yatawezesha dunia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo kwa sasa yamekuwa mwiba kwa mataifa yaliyo masikini na hata tajiri.

Akizungumzia mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ana matumaini makubwa kwa kuwa idadi hiyo ya viongozi inaonyesha utayari wao na kama hiyo haitoshi nchi zaidi ya 180 zimewasilisha mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Ban amesema ni matumaiani yake kuwa COP21 itapitisha mkataba thabiti wa kulenga ustawi wa dunia nzima na kwamba mkataba huo una uhusiano na kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu au ajenda 2030 kwa kuwa..

(Sauti ya Ban)

“Hakuna lengo moja linaloweza kutekelezwa peke yake. Na zaidi ya hapo mabadiliko ya tabianchi, hii ndiyo njia ambayo tunaweza kufanya dunia kuwa bora na salama zaidi na hivi ndivyo tunafanya kazi kwa ajili ya watu.”

Mkutano huo utamalizika tarehe 11 mwezi ujao wa Disemba 2015.