Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia kutumiwa kuinua wanawake kiuchumi: ITC

Teknolojia kutumiwa kuinua wanawake kiuchumi: ITC

Kuelekea maonesho na jukwaa la wanawake wajasiriamali wachuuzi mjini Sao Paulo nchini Brazil mnamo September mosi hadi tatu, shirika la Umoja wa Mataifa la biashara ya kimataifa ITC linajikita katika teknolojia rahisi ya simu za mikononi itakayoinua wanawake kibiashara.

Katika maonesho hayo wanawake takribani 300 watashiriki . Afisa wa ITC Vanessa Erogbogbo ameiambia redio ya Umoja wa Mataifa mikakati anuai itakayotumika katika kuwasaidia wanawake wajasiriamali kuwafikia wanunuzi.

(SAUTI VANESSA)

‘‘Moja ya changamoto kubwa kwa wanunuzi wa kimataifa ni kuwatambua waanwake katika makampuni, kwahiio tumeamua kutumia teknolojia kusaidia kampuni kutambua wanawake wanaomiliki kampuni duniani. ’’

Amesema sekta binafsi imeshirikishwa katika msuala ya uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi na katika kutekeleza hilo ICT imesaini makubaliano na google, ili kujumuisha wanawake kama waajiriwa katika teknolojia.