Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Ceodou Mandingo 'Babuu wa Kitaa' (aliyevaa kofia), Mtetezi wa watu wenye Down Syndrome.
Ceodou Mandingo (Babuu wa Kitaa)

Watoto wenye Down syndrome wana uwezo wakipewa nafasi - Ceodou Mandingo 'Babuu wa Kitaa'

Hii leo katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuhamasisha kuhusu ugonjwa unaothiri uwezo wa mtu kujifunza au Down syndrome tutamsikia Ceodou Mandingo almaarufu Babuu wa Kitaa wa nchini Tanzania ambaye ni mzazi mwenye mtoto aliye na changamoto hiyo na ameikubali hali ya mwanaye na anajitahidi kuelimisha umma kuhusu ugonjwa huo. Kumbuka kuwa mwezi Desemba mwaka 2011, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitia azimio namba (A/RES/66/149) lilitangaza Machi 21 kuwa Siku ya Kimataifa ya Down Syndrome. Maadhimisho ya kwanza yalianza mwaka uliofuata.  

Cabo Delgado, Msumbiji - Rufina akifanyiwa uchunguzi katika kliniki tembezi inayofadhiliwa na UNFPA
© UNFPA Msumbiji/Mbuto Machili

UNFPA na Unitaid zanuia kudhibiti vifo vinavyotokana na kuvuja damu nyingi baada ya kujifungua

Ubia mkubwa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA na la kufanikisha upatikanaji wa dawa na tiba kwa gharama nafuu Unitaid unaofadhiliwa kwa Euro milioni 20 kutoka Muungano wa Ulaya (EU)  kwa ushirikiano na mamlaka za afya barani Afrika, unalenga kuimarisha mifumo ya afya barani Afrika na kuharakisha upatikanaji wa dawa za kuokoa maisha katika harakati kubwa ya kukomesha vifo vinavyotokana na uzazi vinavyoweza kuzuilika.

Watoto katika Ukanda wa Gaza wanapokea chakula huku mahitaji yakiendelea kupungua.
© UNRWA

Chini ya operesheni 1 kati ya 2 za misaada za UN ndizo zimeweza kuingia Gaza Kaskazini mwezi huu

Wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo wamesema chini ya nusu ya misafara ya misaada ya Umoja wa Mataifa iliyopangwa kuelekea kaskazini mwa Gaza eneo lililokumbwa na njaa ndiyo iliyofanikiwa kufikia sasa kwa mwezi huu, licha ya wito wa mara kwa mara kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza misaada kwa zaidi ya watu milioni moja wanaokabiliwa na njaa.