Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulizi jingine la Urusi nchini Ukraine, sheria ya kimataifa ya kibinadamu inapuuzwa - Denise Brown

Msichana mwenye umri wa miaka 13 akipita karibu na majengo yaliyoharibiwa na makombora huko Irpin, Ukraine.
© UNICEF/Filippov

Amani na Usalama

Wiki imeanza na kuendelea kwa mashambulizi katika miji mikubwa ya Ukraine na kuathiri kwa mara nyingine tena raia na miundombinu ya kiraia, amesema leo Denise Brown, Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine. 

Bwana Brown akizungumza kufuatia shambulio la kombora la Urusi lillotekelezwa leo Julai 31 na kulenga nyumba na jengo la chuo kikuu huko Kryvyi Rih, Ukraine amesema Jumuiya ya misaada ya kibinadamu, pamoja na mamlaka za mitaa, “ziko Kryvyi Rih, kusaidia manusura wa shambulio hilo liloharibu majengo ya makazi na miundombinu mingine ya kiraia katika jiji hilo, na kusababisha vifo na majeruhi.”  

Jana timu zetu pia zilitoa msaada wa haraka kwa raia ambao nyumba zao zilishambuliwa huko Dnipro. Uvamizi wa Urusi unaendelea kusababisha uharibifu, na hali inazidi kuwa mbaya kila siku inayopita. Sheria ya kimataifa ya kibinadamu inaendelea kupuuzwa.