Wananchi wa DRC mkitanguliza mazungumzo, matatizo yatakwisha – Meja Jenerali Paul Kisesa
Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli ambaye ni Mkuu wa Utumishi katika Jeshi la Tanzania ametoa wito kwa Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kutanguliza majadiliano katika kutatua matatizo yao ya ukosefu wa amani.