Asilimia 60 ya nchi za kipato cha chini Afrika ziko kwenye mzigo wa madeni:UNCTAD
Takriban asilimia 60 ya nchi za kipato cha chini barani Afrika hivi sasa ziko kwenye mzigo wa madeni, shinikizo kubwa au katika hatari ya kuingia kwenye madeni huku mamilioni ya Waafrika wakitumbukia tena kwenye umasikini wakati huu wakiwa kwenye hatari kubwa ya kutokuwa na uhakika wa chakula, imeonya ripoti mpya ya biashara na maendeleo kwa mwaka 2022 iliyotolewa leo na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD.