Zaidi ya wagonjwa 550 wa Monkeypox wathibitishwa- WHO
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO limesema zaidi ya watu 550 katika nchi 30 wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa Monkeypox ambao huenezwa na virusi vinavyofanana na vile vya ugonjwa wa ndui.