Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hali katika Iraq yatia wasiwasi

KM ameonya kwamba hali ya usalama, kwaujumla, katika Iraq imefikia ‘kikomo cha hatari’ na inabashiria kuzusha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe miongoni ya makundi yenye uhasama wa kimadhehebu nchini humo. Kwa mujibu wa takwimu za Serekali imethibitika kwamba kila siku watu 100 huuawa nchini Iraq na, kwa wastani, 14,000 wengineo hujeruhiwa kila mwezi.

Juhudi za upatanishi juu ya mgogoro wa Uganda ya kaskazini

Serekali ya Sudan karibuni ilijihusisha kwenye mazungumzo ya hali ya juu, yaliyoandaliwa katika mji wa Juba, kwa madhumuni ya kujaribu kuukomesha ule uhasama ulioselelea katika kipindi cha karibu miongo miwili huko Uganda ya kaskazini, kati ya vikosi vya Serekali na wafuasi wa lile kundi la waasi la Lord\'s Resiastance Army (LRA).

Njia za kimagendo katika Ghuba ya Aden

Shirika la UM juu ya Wahamiaji (UNHCR) linabashiria watu wengi watapoteza maisha kutokana na kufumka kwa shughuli hatari za misafara ya magendo ya watu katika Ghuba ya Yemen, umma ambao husafirishwa kutoka Usomali na kupelekwa Yemen.

KM anashtushwa na uhasama wa Eritrea dhidi ya UM

Kufuatia uamuzi wa Serekali ya Eritrea kupiga marufuku na kuwafukuza watumishi watano wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu amelazimika kutoa malalamiko juu ya tabia ya uhasama uliolivaa taifa hilo dhidi ya Shirika la Ulinzi wa Amani la UM Mipakani kati ya Ethiopia na Eritrea (UNMEE), shirika ambalo mtumishi wake mmoja alikamatwa hivi karibuni na Eritrea na kuwekwa kizuizini.

Fafanuzi za FAO juu ya Malengo ya MDGS

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo Duniani (FAO), Bw Jacques Diouf ameonya ya kuwa jumuiya ya kimataifa haitofanikiwa kukamilisha kwa wakati Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) bila ya kukabiliana, kama inavyopaswa, na tatizo liliokithiri la njaa na umaskini.