Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM anashtushwa na uhasama wa Eritrea dhidi ya UM

KM anashtushwa na uhasama wa Eritrea dhidi ya UM

Kufuatia uamuzi wa Serekali ya Eritrea kupiga marufuku na kuwafukuza watumishi watano wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu amelazimika kutoa malalamiko juu ya tabia ya uhasama uliolivaa taifa hilo dhidi ya Shirika la Ulinzi wa Amani la UM Mipakani kati ya Ethiopia na Eritrea (UNMEE), shirika ambalo mtumishi wake mmoja alikamatwa hivi karibuni na Eritrea na kuwekwa kizuizini.