Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Juhudi za Namibia kupta uhuru ilikuwa moja ya agenda ya Umoja wa Mataifa kwa zaidi ya miaka 40. Pichani ni mfanyakazi akimaalizia tangazo la uhuru wa taifa karibu na mji wa Windhoek.
UN Photo/John Isaac

Kukomesha ukoloni sauti za wahusika lazima zisikike:Guterres

Kukomesha ukoloni kumesaidia kubadili uanachama wa Umoja wa Mataifa na kupanua wigo wa wanachama kutoka 51 wa awali na kufikia 193 hivi leo. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza hii leo katika ufunguzi wa mkutano wa kamani maalumu ya Umoja wa Mataifa ya kutokomeza ukoloni mjini New York Marekani.

Lugha mbalimbali
UNESCO

Ni muhimu wazazi wawafunze watoto lugha ya mama-mtangazaji wa lugha ya mama

Katika kuadhimisha  siku ya kimatifa ya lugha ya mama, Umoja wa Mataifai unasema asilimia 43 ya lugha 6000 ambazo zinazungumzwa leo duniani ziko hatarini kutoweka. Na kwamba ni ni mamia kadhaa tu ya  lugha ambazo zimepewa nafasi katika mifumo ya elimu na kutumika kwa umma na ni chini ya lugha 100 ambazo zinatumika katika mtandao wa kidijitali.

Sauti
1'57"
Mwanamke mkazi wa Wau Shilluk Sudan Kusini, mji ambao umeharibiwa na mapigano yaliyosambaratisha makazi, shule na hospitali.
UNICEF/UN0236862/Rich

Vita na ukwepaji sheria lazima vikome Sudan Kusini:UN ripoti

Wakati maelfu ya watu kwa mara nyingine wakifurushwa makwao kwa sababu ya machafuko nchini Sudan kusini , tume ya haki za binadamu kwa ajili ya Sudan Kusini imeitaka serikali ya nchi hiyo na pande zote katika mzozo kuheshimu mkataba wa usitishaji uhasama na kutekeleza mkataba huo mpaya wa amani uliotiwa saini miezi mitano iliyopita.

Sauti
2'25"