Kukomesha ukoloni sauti za wahusika lazima zisikike:Guterres

21 Februari 2019

Kukomesha ukoloni kumesaidia kubadili uanachama wa Umoja wa Mataifa na kupanua wigo wa wanachama kutoka 51 wa awali na kufikia 193 hivi leo. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza hii leo katika ufunguzi wa mkutano wa kamani maalumu ya Umoja wa Mataifa ya kutokomeza ukoloni mjini New York Marekani.

Bwana Guterres amesema kutokomeza ukoloni ni moja ya hatua muhimu sana katika historia ya Umoja wa Mataifa , lakini hadhithi hiyo bado inaandikwa kwani kuna mataifa 17 ambayo bado yanatawaliwa hadi sasa na kila moja la mataifa hayo linahitaji kutupiwa jicho la kina na kuongeza kwamba “ Kila moja bado linasubiri kujitawala na kuwa na serikali yake kwa mujibu wa kipekele cha 11 cha katiba ya Umoja wa Mataifa, ambacho ni azimio la mwaka 1960 kuhusu kutoa uhuru kwa wat una nchi zilizokuwa chini ya ukoloni na pia kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa.”

Hata hivyo amesema katika miezi ya karibuni kumekuwa na hatua zimepigwa hususan kuhusu suala la New Caledonia. Ameongeza kuwa katika kura ya maoni iliyofanyika Novemba mwaka jana , watu wa New Caledonia wameelezea dhamira yao kuhusu mustakbali wao na hali ya taifa lao na kwamba hii ilikuwa hatua muhimu kusonga mbele katika mchakato wa kuondokana na ukoloni kwa mujibu wa azimio la Nouméa la 1998 , ni hatua ya kupongezwa. Kamati hii kwa upande wake iliisaidia New Caledonia katika kipindi cha kuelekea kura ya maoni na ilituma ujumbe mara mbili kwenda katika eneo hilo.

Guterres amesisitiza kwamba Ili kufikia azma ya kutokomeza ukoloni “sauti za watu wa maeneo husika lazima zisikike kama ilivyokuwa kwa New Caledonia, ushirikiano wa pande zote husika ikiwemo watawala ni muhimu, pia ni muhimu kwa watu wa maeneo yasiyojiytawala kuelewa machaguo waliyonayo kuhusu hali yao ya kisiasa na haki ya kuchagua mustakbali wao kwa uhuru.”

Katibu Mkuu pia amepongeza juhudi zinazofanywa na kati hiyo bila kuchoka na kuwasaidia watu wa maeneo yasiyojitawala ili kufikia kuwa na serikali yao. Pongezi hizo pia ni kwa kamati kuhakikisha inaendeleza majadiliano ushirika wenye manufaa kwa watawala na watawaliwa husika.

Guterres amesema mafanikio ya Umoja wa Mataifa katika kutokomeza ukoloni kwa miongo sasa ni ya kututia hamasa sisi sote hivyo “Hebu tutimize wajibu wetu tuwasaidie watu wote katika maeneo yasiyojitawala  katika kukamilishga mchakato wao wa kuondokana na ukoloni kwa mafanikio kwa mujibu wa chaguo lao.”

Kamati hiyo maalumu imezisindikiza nchi nyingi katika safari yake ya kuondokana na ukoloni tangu mwanzoni mwa mika ya 1960 na Katibu Mkuu ameahidi kamati hiyo kwamba Umoja wa Mataifa utafanya kila uwezalo kuunga mkono juhudi na kazi za kamati.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter