Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira bora ni muhimu katika kufikia haki ya kijamii:ILO

Watoto na watu wazima kutoka Romania wakifanyakazi katika eneo la kutupa taka jirani na makazi ya Nadezhda nchini Bulgaria. Familia hizi zinakosa fursa za ajira, ambayo ndio kauli mbiu ya ripoti ya mwaka huu ya ILO kuhusu mtazamo wa ajira na mwenendo Duni
UNICEF
Watoto na watu wazima kutoka Romania wakifanyakazi katika eneo la kutupa taka jirani na makazi ya Nadezhda nchini Bulgaria. Familia hizi zinakosa fursa za ajira, ambayo ndio kauli mbiu ya ripoti ya mwaka huu ya ILO kuhusu mtazamo wa ajira na mwenendo Duni

Ajira bora ni muhimu katika kufikia haki ya kijamii:ILO

Ukuaji wa Kiuchumi

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya haki ya kijamii hii leo, Mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani ILO, Guy Rider amesema ajira bora ni muhimu sana katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu  na haki ya kijamii ambapo bila hivyo amani ya kudumu inakuwa ni ndoto.

Mkurugenzi huo amesema vitu hivyo havikwepeki na kwamba kuna hatua ambayo imepigwa kiuchumi na kijamii, hata hivyo maendeleo hayo na haki haviwani duniani kote akisistiza kwamba

“Watu wengi wameondokana na umasikini , lakini wengi bado wako katika hali duni-Guy Ryder, Mkurugenzi Mkuu wa ILO

“Watu wengi wameondokana na umasikini , lakini wengi bado wako katika hali duni . Wakati teknolojia imesaidia kuzalisha ajira , kufungua njia na fursa na kupunguza baadhi ya shughuli hatarishi, mabilioni ya watu bado leo hii wanahaha kusihi katika uchumi usio rasmi.

Ameongeza kuwa nchi nyingi zimeghubikwa kutokuwepo usawa wa kijamii na kiuchumi au zimesambaratishwa na vita na mizozo. Zaidi ya hapo katika dunia iliyo na mabadiliko ya ajira , ushirika wa kudumu, mila na sheri vimekuwa viukikabiliwa na changamoto na haki za msiki kazini hazitimizwi.

Ujumbe wa Guy Ryder umeongeza kuwa kama ilivyokuwa mwaka 1919 nandivyo ilivyo sasa kwamba amani na utulivu vinaweza kuwa endelevu . Pia amesisitiza kwamba kufikia lengo la ajira zenye hadhi, huru ambazo mtu anachagua, mazirira ya usawa, usalama na utu vitakuwa muhimu sana.

Ameongeza “tunaweza kuchagua njia ambayo itafanya mustakbali bora kuwezekana kwa wanawake na wanaume, kwa familia na jamii kwa ujumla.”

Hakuna maendeleo wala amani bila haki ya kijamii

Kaulimbiu ya Umoja wa Mataifa katika siku hii ya kimataifa ya haki ya kijamii ni: Si mali wala maendeleo bila haki ya kijamii” ILO inasema na huu ndio msingi wa shirika hilo tangu lililipoanzishwa likisisitiza kwa kilatin ‘si vis pacem, cole justitiam- ikimaanisha kwamba Kama unataka amani panda haki.

Kwa karne nzima ILO imekuwa ikifanya kazi kutimiza lengo lake la kuchagiza haki ya kijamii katika ulimwengu wa kazi. Ryder amesema shirika hilo litaendelea kutetea haki na viwango ambavyo vinahimiza ajira zenye hadhi . Pia shirika hilo litachagiza será na mazingira yanayostahili kuundwa kwa kazi zenye hadhi.

Ameongeza kuwa ILO inaahidi kuchagiza majadiliano ili mustakbali bora umuwezeshe kila mtu kuwa na fursa ikiwemo kupitia mazingira endelevu.