Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

DR Congo

Mariam Suleiman, Mkimbizi kutoka DR Congo anayeishi katika makazi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.
UNHCR Video

Wanawake tuna ujuzi, tuna uwezo na tunaweza: Mariam Suleiman

Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Usemi huo unaungwa mkono na mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.

Sauti
2'7"
Hapa ni Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Brazil wanaohudumu kikosi cha kujibu mashambulizi FIB cha MONUSCO wakipatia mafunzo wanajeshi 30 kutoka jeshi la serikali, FARDC j…
MONUSCO/Ado Abdou

DRC: MONUSCO yapatia wanajeshi 30 wa FARDC mbinu za kukabili waasi msituni

Siku zikizidi kuhesabiwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, kuondoka nchini humo, ujumbe huo unaendelea kutekeleza wajibu wake wa kujengea uwezo jeshi la serikali, FARDC kuweza kukabili vikundi vilivyojihami ambavyo vinatajwa kuhusika na asilimia 65 ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwezi Februari mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na serikali. 

Sauti
2'12"