Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 APRILI 2020

21 APRILI 2020

Pakua

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Mashirika ya Umoja wa Mataifa , EU na USAID wamesema janga la virusi vya Corona au COVID-19 limeweka njiapanda mustakbali wa chakula duniani hivyo hatua zinapaswa kuchukuliwa haraka kuepusha baa la njaa

-Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatoa mafunzo likishirikiana na wadau kuhakikisha wakimbizi wanakingwa dhidi ya COVID-19

-Nchini Jordan kwenye kambi ya wakimbizi wa Syria ya Zaa'taar shirika la wakimbizi UNHCR na la elimu sayansi na utamaduni UNESCO wanahakikisha maelfu ya watoto wakimbizi wanapata elimu  kupitia radio, televisheni na simu za mkononi wakati huu ambapo shule zimefungwa kutokana na COVID-19

-Makala yetu leo inatupeleka Uganda utamsikia binti aliyepata mimba akiwa na umri wa miaka 16

-Na Mashinani mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDS Winnie Byanyima ataja mambo matatu ya kuhakikisha waathirika wanalindwa wakati huu wa COVID-19

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
11'24"