Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 APRILI 2020

22 APRILI 2020

Pakua

Leo katika jarida la Umoja wa Mataifa Flora Nducha anakuletea

-Umoja wa Mataifa unasema janga la virusi vya Corona au COVID-19 ni kengele ya kuiamsha dunia kuchukua hatua kulinda sayari hiyo na watu wake  hasa leo ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya mama sayari dunia

- Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na jiji la Nairobi wanachukua hatua kudhibiti kusambaa wa virusi vya corona au COVID-19, kwenye makazi dunia ya Kibera.

-Huko Bangladesh shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR inafanya kila juhudi kuwalinda wakimbizi wa Rohingya kwenye moja ya makazi makubwa zaidi ya wakimbizi duniani ya Cox's Bazaar dhidi ya COVID-19

-Makala leo inatupeleka Geita nchini Tanzania kwa kijana aliyebuni mashine ya kunawa mikono kujikinga na corona bila kushika koki ya kufungua maji bali kwa kutumia miguu kusukuma maji

-Na mashinani tutakuwa Indonesia kwa binti wa miaka 17 Nanda alikeeleza jinsi anavyoendelea na masomo wakati huu wa COVID-19 kupitia mtandao

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Sauti
12'44"