Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Watoto wakimbizi wa Syria katika makazi yasiyo rasmi karibu na Terbol katika Bonde la Bekaa la Lebanon (Aprili 2019)
UNICEF/Siegfried Modola

Hata maji ya kutumia ndani ya familia yanageuka barafu kutokana na baridi kali Lebanon-UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linaendelea kufanya kila jitihada kuwasaidia wakimbizi na raia wa Lebanon ambao wanakabiliana na  moja ya misimu yenye baridi kali zaidi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 10, huku theluji ikidondoka katika maeneo ambayo hayajashuhudia theluji kwa muongo mmoja. 

Sauti
2'