Ethiopia

Tigray Ethiopia, WFP yatangaza kipaumbele chake

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limekaribisha kusainiwa kwa makubaliano ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za kibinadamu ambazo hazina kizuizi, endelevu na salama kwa maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Serikali ya Shirikisho katika mkoa wa Tigray na maeneo yanayopakana na mikoa ya Amhara na Afar. 

UNHCR iko tayari kuanza tena utoaji wa misaada kwa waliofurushwa Tigray 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, liko tayari kuanza tena shughuli zake kamili za kibinadamu katika mkoa wa Tigray, Ethiopia mara tu hali itakaporuhusu, kufuatia makubaliano ya kurejesha upatikanaji, ameeleza hii leo msemaji wa shirika hilo Babar Baloch katika mkutano wake na vyombo vya habari mjini Geneva Uswisi.  

UNHCR yaitaka Ethiopia kuruhusu kufikiwa wakimbizi 96,000 wasio na chakula Tigray

Shirika la Umoja wa Mastaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limeiomba serikali ya Ethiopia kulipa ruhusa ya dharura ili kuweza kuwafikia wakimbizi 96,000 kutoka Eritrea waliokwama kwenye jimbo la Tigray ambao sasa hawana huduma muhimu ikiwemo chakula kutokana na machafuko yanayoendelea kwa mwezi mmoja sasa. 

Wakimbizi wa Ethiopia sasa ni zaidi ya 43,000, Mkuu wa UNHCR atembelea Kartoum Sudan kutathimini hali.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi yuko ziarani nchini Khartoum, Sudan kuangazia hali ya wakimbizi wa Ethiopia ambao hadi sasa zaidi ya 43,000 wameingia mashariki mwa Sudan wakitokea jimbo la Tigray.  

Tishio la mapigano zaidi Mekelle, Ethiopia, linaweka maisha ya watoto hatarini- Henrietta Fore 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limezisihi pande zote kinzani katika mgogoro nchini Ethiopia kuwaepusha watoto na athari za uahasama katika jimbo la Tigray.

Idadi ya wanaokimbia Tigray Ethiopia kuingia Sudan sasa imezidi 40,000: UNHCR 

Wakati idadi ya watu wanaokimbia jimbo la Tigray nchini Ethiopia kuingia mashariki mwa Sudan sasa imezidi 40,000, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linafanya jitihada kupata msaada wa kutosha unaohitajika kwa watu hao walio katika uhitaji mkubwa. 

UN yakaribisha uteuzi wa wajumbe watatu AU kwa ajili ya kutatua mzozo wa Ethiopia 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerkaribisha hatua ya jana Ijumaa ya Muungano wa Afrika AU, ya uteuzi wa wajumbe watatu wa ngazi ya juu ili kusaidia juhudi za kusaka suluhu ya amani ya mgogoro wa jimbo la Tigray nchini Ethiopia. 

Mashirika ya UN yaelezea hofua yake kutofikia wakimbizi 100,000 Tigray, Ethiopia

Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la mpango wa chakula duniani WFP na la kuhudumia Watoto UNICEF, leo yameelezea hofu yake ya kushindwa kuwaf

Sauti -
2'42"

Tunahofia kushindwa kufikisha msaada kwa maelfu ya wanaouhitaji Tigray Ethiopia:WFP/UNICEF 

Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la mpango wa chakula duniani WFP na la kuhudumia Watoto UNICEF, leo yameelezea hofu yake ya kushindwa kuwafikia wakimbizi 100,000 wakiwemo watoto katika jimbo la Tigray Ethiopia kwa misaada muhimu ya kuokoa maisha ikiwemo chanjo na elimu.

Ninaumia kwa kinachoendelea nyumbani Ethiopia siwezi kuegemea upande wowote:Dkt.Tedros 

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema anaumia na kupata uchungu mkubwa moyoni kufuatia hali ya machafuko inayoendelea Ethiopia nchi anakotoka ,na amertoa wito kwa pande zote katika mzozo kufanya kila liwezikanalo kwa ajili ya kurejesha amani na kuhakikisha ulinzi wa raia na pia kutoa fursa za huduma za afya na misaada ya kibinadamu kwa wale wanao ihitaji.